NAIBU Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Maryprisca Mahundi ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya na Mkurugenzi wa Maryprisca Women Empowerment Foundation (MWEF) ametekeleza ahadi yake kwa wafungwa na mahabusu katika Gereza la Ruanda Jijini hapa kwa kukabidhi vifaa vya michezo.
Vifaa vya michezo vilivyokabidhiwa ni pamoja na mipira na seti mbili za sare na tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 5000.
Mhandisi Mahundi amekabidhi msaada huo leo Septemba 27,2024 na kuhaidi kuendelea kuwaunga mkono Kwa kuwanunulia magodoro pamoja na ujenzi wa bweni kwa ajili ya wafungwa wanawake.
Kwa upande wake Mkuu wa Gereza la hilo Kamishina Msaidizi Sinjonjo Mwakyusa ameishukuru Taasisi ya Maryprisca Women Empowerment Foundation pamoja na Ofisi ya Mbunge Mhe. Mahundi kwa msaada alioutoa nakueleza kuwa utasaidia kuimarisha afya za wafungwa na mahabusu waliopo katika gerezani hilo.
Mwakyusa ameshukuru Mhandisi Mahundi kwa msaada huo kwani utaleta tabasamu kwa wafungwa hususani vifaa vya michezo.
0 Comments