John Mongella, Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, akizungumza na viongozi wa mashina na matawi ya CCM katika Halmashauri ya Msalala, mkoani Shinyanga. Mongella, ambaye pia ni mlezi wa chama kwa mkoa huo, yupo katika ziara ya siku saba inayolenga kukagua uhai wa chama na kuhakikisha utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2024. Kesho, ataendelea na ziara yake katika Halmashauri ya Ushetu, ambako atafanya vikao vya ndani na vya hadhara kwa lengo la kuimarisha chama. 07/9/2024
0 Comments