Rais Samia Mgeni Rasmi Kilele Cha Miaka 60 Ya Jeshi La Polisi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na amiri jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Daktari Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Kilele cha Miaka 60 ya Jeshi la Polisi inayofanyika katika shule ya Polisi Tanzania Moshi Mkoani Kilimanjaro septemba 17,2024.

Akitoa taarifa hiyo leo septemba 16,2024 Moshi Mkoani Kilimanjaro Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna wa Polisi DCP David Misime amesema kuwa awali Jeshi hilo lilitoa taarifa kuhusiana na maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Polisi Tanzania nakufanyika shughuli mbalimbali katika Mikoa na vikosi vya Jeshi hilo hapa nchini.

DCP Misime ameongeza kuwa shughuli hizo ni pamoja nakupima afya wananchi bure katika Hosptali Kuu ya Jeshi hilo iliyopo Barabara ya kilwa (kilwa Road) Jijini Dar es Salaam na Zahanati zote za Jeshi zilizopo Mikoa yote.

Sambamba na hilo amebainisha kuwa mambo mengine yaliyofanyika katika maadhimisho hayo ni Pamoja na Jeshi la Polisi kushirikiana na Jamii katika michezo Pamoja na kutoa elimu juu ya kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu katika mikoa mbalimbali hapa nchini.

Vilevile ameweka wazi kuwa ulifanyika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi ambao umemalizika siku ya Jana Septemba 15,2024 huku akibainisha kuwa Septemba 17,2024 Jeshi hilo linatarajia kuhitimisha kilele cha maadhimisho hayo katika Shule ya Polisi Tanzania Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Pia amesisitiza kuwa maadhimisho hayo yataambatana na tuzo na zawadi kwa askari ambao wamelitumikia Jeshi la Polisi kabla na baada ya uhuru huku akiweka wazi kuwa maandalizi yamekamilika na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari Samia Suluhu Hassan.



TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments