Akizungumza jijini Arusha Dkt.Mpango amesema kuwa kupitia mchango iliodhamiriwa kitaifa wa Tanzania imeweka mbele malengo ya kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama vijijini na mijini kutoka asilimia 86 na 67.7 mwaka 2020 hadi asilimia 100 ifikapo mwaka 2030 ambapo amesema uchafuzi wa mazingira kwa silimia kubwa husababishwa na matumizi ya kuni na mkaa na sababu kuu ya matatizo ya kiafya.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazinhira Dkt. Ashatu Kijaji amesema nchi ya Tanzania imejitoa katika kikabiliana na mabadiliko ya tabianchi kupitia mipango na sera mbalimbali ikiwemo sera ya taifa ya mazingira ya mwaka 2021, Mpango mkuu wa mazingira wa kitaifa wa miaka ya mkakati kutoka 2022 hafi 2032 na serq ya taifa ya uchumi wa bluu ya mwaka 2024 .
Dkt. Kijaji ameeleza kuwa ili kuboresha hatua za hali ya hewa ,Tanzania inatafuta ushirikiano na washirika wa maendeleo katika kuimarisha uimara wa hali ya hewa katika maeneo yaliyoathirika na mafuriko, kukuza teknolijia za kupikia safi na nishati safi, kutekeleza usimamizi endelevu wa ardhi katika maeneo yaliyokabiliwa na maporomoko ya ardhi pamoja na kutekeleza mbinu endelevu za usimamizi wa takataka ngumu katika miji mikubwa.
Awali akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Monduli Festo Kiswaga pamoja na kuwahakikishia usalama wa kutosha na upatikanaji wa huduma zote muhimu kwa washiriki wa jukwaa hilo na mkutano huo amesema mkoa wa Arusha ni miongoni mwa mikoa ambayo iliyokumbwa na athari za mabadiliko ya tabianchi
Chanzo Matukio Daima Media
0 Comments