TIMU ya Pamba Jiji inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara imeamua kuachana na Kocha Mkuu klabu hiyo Goran Kopunovic.
Taarifa ya Pamba Jiji iliyotolewa na Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu Ezikiel Ntibikeha leo imesema pia klabu hiyo imefikia makubaliano ya kusitisha mikataba ya wasaidizi wa Kopunovic, Salvatory Edward, Kocha wa magolikipa Razack Siwa na kocha wa viungo Circus Kakooza.
“Uongozi wa klabu ya Pamba Jiji FC unautaarifu umma kuwa umefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu Goran Kopunovic,” imesema taarifa hiyo.
SOMA: Pamba Fc wazindua tawi sengerema
Pamba Jiji iliyopanda daraja Ligi Kuu msimu huu imesema kwa sasa timu hiyo itakuwa chini ya Kocha Mathias Wandiba aliyekuwa kocha wa timu ya vijana chini ya miaka 20 hadi hapo atakapotangazwa kocha mkuu.
Goran Kopunovic alitangazwa kuwa Kocha Mkuu wa Pamba Jiji Julai 15, 2024 kwa kandarasi ya mwaka mmoja.
0 Comments