NCHIMBI ‘AFUNGA’ OFISI ZA CHADEMA ITILIMA.

 Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Itilima, Katibu na wanachama wao wahamia CCM.


Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, Ndugu Terry Kilugala, na Katibu wake wa Wilaya ya Itilima, Ndugu Gershom Migasa Mipawa, pamoja na wanachama wao zaidi ya 60, wamehamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kupokelewa na Katibu Mkuu wake, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Luguru, wilayani Itilima.

Ndugu Kilugala, akizungumza kwenye mkutano huo, amesema mbali na Chadema kuwatumia vibaya viongozi na wanachama wake, kisha kuwaacha ‘watupu’ wakiangaliana wenyewe kwa wenyewe, uongozi wa CCM na utendaji kazi wa serikali yake, chini ya Mwenyekiti wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, vyote vimemfanya arudi nyumbani.

“Tulikuwa tunaenda Mwanza siku mbili kwa ubovu wa barabara, leo tunaenda na kurudi. Lazima tuseme ukweli, CCM imefanya kazi, lakini wenzetu wamebakia kusema uongo na kututumia vibaya.



TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments