DIWANI SIMANJIRO APONGEZA UFAULU MZURI

DIWANI wa Kata ya Endiamtu Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Lucas Chimbason Zacharia amewapongeza walimu wa shule za msingi za eneo hilo kwa kufanikisha ufaulu mzuri kwa wanafuniz wa darasa la saba.


Luka ameyasema hayo kwenye kikao cha Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilay aya Simanjiro kilichofanyka mji mdogo wa Orkesumet, yalipo makao makuu ya wilaya hiyo.

Amesema walimu wa shule za msingi za kata hiyo wamejitahidi kufundisha vyema wanafunzi wao hadi kupata ufaulu mzuri na kufanikiwa kujiunga na shule za sekondari kwa kidato cha kwanza mwaka ujao wa 2025.

“Niwapongeze walimu wa shule za msingi kwa ufundishaji mzuri na kusababisha wanafunzi wa darasa la saba wanaosoma kwenye kata ya Endiamtu kufaulu vyema,” amesema Luka.

Amesema wanafunzi wa darasa la saba wa shule za msingi kwenye kata yake za Glisten, New Light, Kazamoyo, Mirerani, Jitegemee na Endiamtu, wamefaulu vyema na kujiunga na sekondari.

Diwani wa kata ya Mirerani Salome Nelson Mnyawi amesema miongoni mwa miradi iliyofanyika kwenye kata yake ni ujenzi wa kituo cha afya japo kuna changamoto zinazowakabili.

Salome amezitaja baadhi ya changamoto hizo ni barabara za ndani hasa zinazokwenda kwenye taasisi ikiwemo shule, uzio machinjioni, mageti ya soko na mnada getini na ubadilishaji wa matumizi ya shilingi milioni 5 za ukarabati vyoo.


Diwani wa kata ya Loiborsiret, Ezekiel Lesenga (Mardadi) amesema eneo hilo linakabiliwa na ubovu wa barabara ya kutoka Narakauo hadi Emboreet na barabara ya Orkiringo hadi mtoni, kivuko kiwekwe wanapata tabu mvua ikinyesha.


Mardadi amesema zahanati ya kijiji cha Kimotorok inapaswa kumalizika ili jamii ya eneo hilo iweze kupata matibabu kwa ukaribu zaidi katika kijiji chao.


Diwani wa viti maalum Tarafa ya Msitu wa Tembo, Neema Sinjori ameiomba mamlaka ya maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) Wilaya ya Simanjiro kukarabati kisima cha Olchoronyori ili wapate maji kwani awali walionjeshwa.

Dwani wa Kata ya Endiamtu Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Lucas Chimba Zacharia, amewapongeza walimu wa shule za msingi wa Kata hiyo kwa kufaulisha vyema wanafunzi wa darasa la saba waliohitimu kwenda sekondari pia amezungumzia juu ya changamoto ya umaliziaji maabara ya shule ya sekondari Mirerani B.W.Mkapa na ujenzi wa korido ya kituo cha afya Mirerani eneo la kuhifadhi miili ya marehemu.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments