KAMATI YA USTAWI NA MAENDELEO YA JAMII YAIPONGEZA NSSF UWEKEZAJI WENYE TIJA DARAJA LA KIGAMBONI

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeupongeza Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii – NSSF kwa uwekezaji wenye tija katika mradi wa Daraja la Mwalimu Nyerere lililopo Kigamboni.


Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Fatma Toufiq leo Novemba 11, 2024 Jijini Dar es salaam wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya miradi inayotekelezwa na NSSF likiwemo Daraja la Mwalimu Nyerere na mradi wa Dege Village.

“Tunaipongeza NSSF kwa kazi nzuri wanayoifanya katika daraja la Mwalimu Nyerere, na ule ni mfano wa kuigwa katika kubuni utaratibu kufanya malipo kielektroniki katika   ukusanyaji pesa” amesema.

Aidha, Mhe. Fatma ameushauri Mfuko huo kuanzisha mfumo wa malipo ya kabla(Pre paid) darajani hapo  ili kupungunza msongamano wa magari na kurahisisha ukusanyaji wa mapato.

Akizungumza awali, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete ameitaka menejimenti ya NSSF kutoa elimu kwa madereva na wamiliki wa magari kuhusu faida ya kutumia mfumo wa kielektroniki wakati wa kupita darajani hapo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Masha Mshomba, amesema moja ya mafanikio ya mradi huo ni kuongezeka kwa mapato kufikia Bilioni 18.72 kwa mwaka wa fedha 2023/2024.









TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments