TANZANIA YAFUZU AFCON 2025

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imefanikiwa Kufuzu kucheza Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) ambayo inatarajiwa kufanyika Nchini Morocco.

Goli pekee la Simon Happygod Msuva limeiwezesha Tanzania kupata ushindi wa Goli 1-0 dhidi ya Guinea kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam
Kwa ushindi huo, Taifa Stars inafikisha pointi 10 baada ya mechi zote sita za kundi hilo na kuungana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) yenye pointi 12 za mechi tano kufuzu AFCON ya mwakani.

Guinea inabaki na pointi zake tisa baada ya mechi zote sita za kundi katika nafasi ya tatu, mbele ya Ethiopia yenye pointi moja katika mechi tano.

Mechi ya mwisho ya Kundi H DRC wanamenyana na Ethiopia tangu Saa 1:00 usiku Uwanja wa Martyrs de la Pentecôte Jijini Kinshasa.

Hii inakuwa mara ya nne kihistoria Tanzania kufuzu AFCON baada ya mwaka 1980 nchini Nigeria, 2019 Misri na 2023 nchini Ivory Coast na mara ya kwanza kufuzu Fainali mbili mfululizo.

Ikumbukwe kwa tiketi ya uenyeji wakishirikiana na Kenya na Uganda – Tanzania pia watacheza Fainali za AFCON za mwaka 2027.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments