WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUCHANGIZA URITHI WA UTAMADUNI USIOSHIKIKA KUCHOCHEA AJIRA KWA WANAWAKE NA VIJANA

Waandishi wa Habari wa redio jamii Mkoani Katavi wametakiwa kuchagiza urithi wa utamaduni usioshikika ili kuchochea fursa za ajira kwa Wanawake na vijana.

Carol Steven, Afisa Michezo, Utamaduni na Vijana Mkoani Katavi ametoa wito huu leo wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari wa redio jamii Mkoani humo.

Mafunzo hayo yameandaliwa na shirika la Tanzania Media for Community Development kwa ufadhili wa mradi wa UNESCO- Alwalweed Philanthropies ili kujenga uwezo wa kutumia taaluma zao ili kuchagiza utamaduni wa urithi usioshikika na kuchochea fursa za ajira kwa Wanawake na vijana Mkoani Katavi.

Bwana Steven alisisitiza kuwa nchi ya Tanzania ni nchi ya kipekee ambayo imeendelea kulinda utamaduni wake na kusisitiza kuwa mafunzo hayo yamekuja kwa wakati muafaka kwani Mkoa wa Katavi una fursa nyingi zinazohitaji kutangazwa.

Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Leah Gawaza aliwataka waaandishi hao kutangaza urithi wa utamaduni usioshikika ili kuvutia wawekezaji Mkoani na kutengeneza fursa za kiuchumi kwa Wanawake na vijana,

“ Ukimsaidia Kijana umesaidia taifa la kesho na ukimsaidia mwanamke umeisaidia jamii nzima,” alisema Gawaza ambae alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mhe. Jamila Kimaro.

Mkoa wa Katavi ni moja wa mikoa mitano inayosifika na kuongoza kwa uzalishaji wa chakula ambapo pia ina vivutio vingi vya utalii na madini.

Mafunzo hayo pia yamejumuisha wasanii kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma.









TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments