WAKILI MKUU WA SERIKALI AKUTANA NA RAIS WA MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU NA WATU JIJINI ARUSHA

 

Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi akimkabidhi Jarida la Wakili Mkuu Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Mhe. Jaji Imani Aboud alipotembelea Mahakama hiyo kwa lengo la Kujitambulisha na kuona namna Mahakama hiyo inavyotekeleza majukumu yake Jijini Arusha.
Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt Ally Possi (wa nne kushoto) na ujumbe wake akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Mhe. Jaji Imani Aboud (wa nne kulia) baada ya kutembelea Mahakama hiyo kwa lengo la kujitambulisha na kujionea namna Mahakama hiyo inavyotekeleza majukumu yake jijini Arusha.
Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi akifafanua jambo kwa Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Mhe. Jaji Imani Aboud (hayupo pichani)  alipotembelea Mahakama hiyo kwa lengo la kujitambulisha na kuona namna inavyofanya kazi jijini Arusha.
Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Mhe. Jaji Imani Aboud akizungumza na Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi na ujumbe wake (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kujitambulisha na kuona namna Mahakama hiyo inavyofanya kazi jijini Arusha
Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi (aliyeketi mbele kushoto) akizungumza na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Mhe. Jaji Imani Aboud (aliyeketi kushoto kwake) alipofika Mahakamani hapo kujitambulisha na kuona namna inavyofanya kazi jijini Arusha

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments