MEYA WA JIJI LA ARUSHA AZINDUA MITAMBO YA UKARABATI WA BARABARA YENYE THAMANI YA BILIONI 1.7


 Na Pamela Mollel Arusha 

Mstahiki Meya Jiji la Arusha Mhe Maxmillian Matle Iranqhe amezindua mitambo Mipya ya ujenzi na ukarabati wa barabara za ndani zilizo chini ya Usimamizi wa Jiji la Arusha zilizogharimu bilioni 1.7

Aidha barabara hizo ni mbazo zipo chini ya TARURA kwa lengo la kuhakikisha barabara za ndani zinakiwango kizuri kwa wananchi kutumia katika shughuli zao za kila siku

Katika hafla hyo Mitambo iliyozinduliwa ni pamoja na mtambo wa  greda moja na malori makubwa mawili

Akizungumza katika uzinduzi huo jijini Arusha Meya Maxmillian,anawakumbusha watendaji kuhakikisha wanatunza mitambo hiyo ili iweze kufikia Malengo kusudiwa

Pia aliwataka Waheshimiwa Madiwani wa Jiji la Arusha kuhakikisha wanahamasisha wananchi kushiriki shughuli za usafi wa mitaa ili Wageni wanaotembelea jiji la Arusha wavutiwe zaidi 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Arusha John Kayombo amepongeza hatua hiyo ya upatikanaji wa mitambo hiyo ambayo inakwenda kutatua changamoto katika barabara za ndani wanazotumia wananchi

Aliongeza kuwa moja ya changamoto walizokutana nazo Madiwani wake ni pamoja na kuburuzwa katika tope kutokana na ubovu wa barabara ambapo amekiri hali hiyo kutojitokeza tena.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments