Napoli: Punguzeni bei ya Garnacho, mtampata Osimhen

 TETESI za usajili zinasema klabu ya Napoli imeipa Manchester United ofa ya punguzo la bei kwa ajili ya mshambuliaji Victor Osimhen wa klabu hiyo ya Italia anayecheza Galatasaray kwa mkopo ikiwa Mashetani hao Wekundu watakubali kupunguza bei ya winga Alejandro Garnacho. (Il Mattino – Italia)

WINGA WA MANCHESTER UNITED, ALEJANDRO GARNACHO.

Nottingham Forest imepanga mshambuliaji wa Wolves na Brazil, Matheus Cunha, kuwa mlengwa wake mkuu wa dirisha la usajili mwezi huu katika harakati za kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya. (Mail)

Pia Arsenal imeonesha nia kumsajili Cunha mwenye umri wa miaka 25 wakati dirisha la usajili Januari. (Fichajes)Hakuna ofa zozote zilizowasilishwa kwa ajili ya Cunha na Wolves ina matumaini kwamba asaini mkataba mpya wa muda mrefu. (Express and Star)

Chelsea inatarajiwa kufanya mazungumzo zaidi na Manchester United kuhusu winga wa Argentina, Alejandro Garnacho, mwenye umri wa miaka 20, anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 50. (Telegraph)

Winga wa Manchester United na timu ya taifa ya Brazil Antony, 24, anakaribia kukamilisha uhamisho Kwenda Real Betis kwa mkopo. (Sky Sports)

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments