RAIS SAMIA ASHIRIKI MKUTANO WA DHARURA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI WA ASASI YA SIASA, ULINZI NA USALAMA SADC-ORGAN

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-Organ) Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi hiyo uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Januari, 2025.

Katika Mkutano huo, Mhe. Rais Dkt. Samia alishiriki pamoja na Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Hakainde Hichilema sambamba na Rais wa Jamhuri ya Malawi Mhe. Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera. Aidha, Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mhe. Felix Antoine Tshisekedi walishiriki kwa njia ya mtandao.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments