TAASISI YA MAMA ONGEA NA MWANAO YAFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI GWAJIMA

 TAASISI ya Mama Ongea na Mwanao imefanya mazungumzo na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Makundi Maalumu, Dkt. Dorothy Gwajima ambapo ameahidi kutoa ushirikiano kwa taasisi hiyo ambayo ipo chini ya Mwenyekiti wake Steven Nyerere.


Akizungumza mara baada ya kufanya mazungumzo, Steven Nyerere amesema kuwa Waziri Gwajima anatambua umuhimu wa Wanawake hasa kulinda utamaduni wetu na kukikumbusha kizazi hiki kulinda amani na kukemea vitu mbalimbali vinavyovunja utu.

Amesema kuwa "Dkt. Gwajima anatambua mchango wetu, kuanzia kampeni ya Samia nivushe kiatu, baiskeli ya mama na makundi ya walemavu".

Aidha amesema kuwa Kuelekea kilele cha siku ya wanawake duniani mwezi Machi taasisi ya mama ongea na mwanao itatoa ushirikiano mkubwa kuhakikisha jambo la mama ni jambo letu.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments