WANANCHI NA VIONGOZI MKOANI SINGIDA WAUNGA MKONO RAIS DR. SAMIA KUWA MGOMBEA URAIS 2025

Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Singida BERTHA NAKOMOLWA amesema Rais Dkt SAMIA SULUHU HASSAN ameleta maendeleo makubwa katika kipindi chake kifupi na hivyo ni vizuri aendelee kuliongoza taifa hili ili wananchi wapate maendeleo makubwa zaidi.

NAKOMOLWA alisema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Maluga wilayani Iramba akiwa katika ziara yake ya kuelekea sherehe za maadhimisho ya kuanzishwa kwa Chama cha Mapinduzi CCM Tarehe 5/2/1977.

Alisema Chama hakiwezi kubadili Rais kwani Rais Dkt SAMIA SULUHU HASSAN anatosha na anafaa kuendelea kuliongoza taifa kwa kipindi kingine cha miaka mitano ili aweze kuwaletea wananchi maendeleo.

Akiwa katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata hiyo ya Maluga wilayani Iramba, Wananchi waliomba serikali kuiboresha Zaharani ya Kata hiyo ambayo inakabiliwa na changamoto mbalimbali hali inayosababisha kufuta huduma Singida mjini, ambapo ni mbali.

Wananchi hao walisema Zahanati hiyo inakabiliwa na upungufu wa wahudumu wa afya na Vifaa Tiba, hivyo waiomba Serikali kuwaongezea wahudumu hao ili waweze kupata huduma za afya zilizobora na waache kwenda mbali kufuata huduma.

Lakini pia waomba kujengewa Wodi ya wazazi ili akina Mama wajawazito wasipate changamoto wakati wa kujifungua.

Akitolea majibu kuhusu Zahanati hiyo, Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi CCM Mkoa wa Singida BERTHA NAKOMOLWA alisema changamoto hiyo ameichukua na ataiwasilisha kwa viongozi ili iweze kutatuliwa na wananchi waanze kupata huduma za afya katika Zahanati hiyo.

NAKOMOLWA alisema atashirikiana na Mbunge wa jimbo hilo na uongozi wa Mkoa ili juhudi za kuanza ujenzi zianze na kupeleka Vifaa Tiba kwa lengo la kutatua changamoto zilizopo hapo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments