Aston Villa wakamilisha usajili wa Rashford

 

Aston Villa wanakaribia kukamilisha usajili wa mshambuliaji Marcus Rashford kutoka Manchester United.

Rashford anajiunga na Villa kwa mkopo wa miezi mine hadi Juni. Kwa mujibu wa taarifa ya mwandishi wa habari za usajili nchini Italia, Fabrizio Romano asilimia 70 ya mshahara wa Rashford utatolewa na Villa huku United ikitoka asilimia 30.

Mkopo huo una kipengele cha Rashford kuuzwa moja kwa moja Villa Park kwa uhamisho wa pauni milioni 40 kwa mkataba wa miaka mitatu na nusu. Villa wameomba vipimo vya afya vifanyike leo.

Villa wamemuuza mshambuliaji Jhon Durán kwenda Al-Nassr huku kukiwa na tetesi huenda Ollie Watkins akatimka pia, licha ya kocha wa Villa, Unai Emery kudai mwingereza huyo hauzwi. Villa pia wanakaribia kumnasa Marco Asensio kutoka PSG.

Dirisha la usajili linafungwa kesho saa 6 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments