Naibu Waziri Asema Serikali Ya Tanzania Inaendelea Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Stanslaus Nyongo (Mb.), amebainisha kuwa Serikali ya Tanzania, chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inaendelea kufanya mabadiliko makubwa katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji.


Mhe. Nyongo aliyasema hayo Februari 11, 2025, jijini Dar es Salaam, alipokuwa akifungua Kongamano la nne la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Italia.

Miongoni mwa hatua hizo ni pamoja na kurekebisha sheria za biashara, kufuta ada, tozo, na faini ambazo hapo awali zilikuwa kikwazo kwa wafanyabiashara.

Katika hotuba yake, Mhe. Nyongo aliwahamasisha wawekezaji kutoka Italia kuwekeza nchini Tanzania akisisitiza kuwa ni mahali sahihi kwa uwekezaji barani Afrika.

Aidha, katika kongamano hilo, Mhe. Nyongo alishuhudia utiaji saini wa Makubaliano ya Ushirikiano (Memorandum of Understanding) kati ya
 Chuo Kikuu cha Taifa cha Muhimbili na Chuo Kikuu cha Rome, ikilenga kuimarisha utafiti na afya.



TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments