NAIBU WAZIRI MWINJUMA "ASISITIZA TAARIFA SAHIHI WAKATI WA UCHAGUZI"

 

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mwinjuma Muumini akizungumza wakati akifunga Mkutano wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji Tanzania ' Annual Broadcasters' Conference' katika ukumbi wa New Generation Jijini Dodoma.


Mkutano huo wa siku mbili (Februari 13 na 14,2025) umeandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ukishirikisha Vituo vya utangazaji, waandaaji na wasambazaji wa maudhui mtandaoni, wauzaji wa vifaa vya utangazaji na wadau wote wa sekta ya utangazaji unaongozwa na kauli mbiu 'Wajibu wa vyombo vya utangazaji kuelekea uchaguzi mkuu 2025'. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

NAIBU Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma, amewasisitiza waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi za uchaguzi Mkuu 2025,wa kuchagua Madiwani,Wabunge na Rais.

Amebainisha hayo leo Februari 14,2025 wakati akifunga mkutano wa mwaka wa vyombo vya utangazaji nchini, Jijijini Dodoma, ulioandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambao umedumu kwa muda wa siku mbili.

Amesema kupitia mafunzo hayo anaamini waandishi wamejifunza mambo mbalimbali ya kitaaluma, na kwamba yamewajenga hasa kwenye utoaji wa taarifa sahihi hasa katika kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa 2025.

"vyombo vya habari ni muhimu sana kuelekea kwenye uchaguzi kuu wa mwaka huu, na msipotoa taarifa sahihi mnaweza kuchangia demokrasia kuzama,"amesema Mwinjuma.

"Hivyo nawasihi mtoe taarifa sahihi,  zisizoegemea upande wowote, na mhabarishe umma ili wafanye machaguo sahihi kwa kuchagua viongozi wanaowataka,"ameongeza.

Amesisitiza pia suala la matumizi ya lugha sahihi ya kiswahili katika utangazaji, ili kuilinda lugha hiyo na kutokubali kuharibiwa, bali waitumie kwa ufasaha.

Aidha,amesema serikali ipo pamoja na sekta ya habari,na kwamba milango ya Wizara ipo wazi, na kusisitiza dhamira ya Rais Samia suluhu Hassani ni kuikuza Sekta hiyo,na ndiyo maana alipoingia Madarakani alivifungilia vyombo vya habari ambavyo vilikuwa vimefungiwa.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Andrew Kisaka, naye amesisitiza waandishi wa habari wawe makini wanapo ripoti habari za uchaguzi na kutoongeza "Chumvi", pamoja na kutoa uwiano sawa wa muda wa vipindi kwa wagombea.

Amesema mikutano hiyo wameianzisha TCRA,kwa malengo ya kukuza sekta ya utangazaji

Kauli mbiu ya Mkutano huo inasema "wajibu wa vyombo vya utangazaji kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.




TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments