Rais Samia ametimiza, aungwe mkono -Hapi

KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Taifa, Ally Hapi, (MNEC) ameandika historia wilayani kwa kupokelewa na kufanya mkutano na wananchi eneo la Mpwapwa Mjini tukio ambalo halijawahi kufanyika kwa ukubwa huo katika miaka ya karibuni.

Hapi amefanya mkutano katika uwanja wa Mnara wa Mashujaa, ambapo wananchi walijitokeza kwa wingi kumsikiliza ikiwa ni sehemu ya ziara yake wilayani humo.

Akihutubia umati huo, ameeleza mafanikio makubwa ya serikali ya Rais  Samia Suluhu Hassan akisisitiza kuwa serikali imeendelea kutekeleza miradi mingi ya maendeleo kwa ufanisi mkubwa ikiwemo kujenga shule mpya za msingi 18, sekondari 13,  madarasa mapya ya shule za msingi 280 na madarasa mapya ya sekondari 313.

Aidha, mafanikio mengine aliyotaja Hapi ni ujenzi wa vituo vipya vya afya 5, zahanati 10, umeme vijiji 108 kati ya 113 yote yakiwa yamefanyika katika kipindi cha uongozi wa  Samia Suluhu Hassan.

Ziara hiyo imehudhuriwa na viongozi wa chama, jumuiya na serikali wilaya na mkoa wakiwemo mbunge wa Mpwapwa Mhe. George Malima na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, George Boniphace Simbachawene ambaye ni mbunge wa Kibakwe.

Imetolewa na Idara ya Oganaizesheni ya Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments