Rais Samia “msiwaogope wapinzani”

                           

RAIS Samia Suluhu Hassan, amekitaka Chama cha Mapinduzi kutoruhusu kunyemelewa na kiburi cha kuwabeza wapinzani na kutoingiwa na pepo la kuwaogopa, bali waendelee kulinda heshima na imani waliyopewa na wananchi ya kuliongoza Taifa, huku akiwasihi viongozi kutobweteka kwasababu CCM ni chama kikubwa.

Rais Samia ambaye pia ni mgeni rasmi katika kilele cha Maadhimishi ya miaka 48 ya CCM, ameyasema hayo leo Februari 5, 2025 katika maadhimisho hayo yaliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, ambapo amesema kutokana na Chama cha Mapinduzi kutekeleza ahadi zake tangu mfumo wa vyama vingi uanze, wananchi wa Tanzania wameendela kukipa dhamana chama hicho kuongoza Taifa katika pande zote mbili za muungano.

“CCM inatekeleza ahadi zake tangu mfumo wa vyama vingi urejeshwe nchini. Miaka 33 iliyopita wananchi wa Tanzania wameendelea kukipa dhamana Chama cha Mapinduzi kuliongoza Taifa letu katika pande zote mbili za muungano pamoja na hali hiyo ‘Tusibweteke’.”

“Tunatimiza miaka 48 katika mwaka wenye vuguvugu la uchaguzi mkuu nchini, kama nilivyosema kwenye mkutano mkuu maalumu uliomalizika hivi karibuni tusiruhusu kunyemelewa na kibri cha kuwabeza wapinzani wetu lakini pia tusiingiwe na pepo la kuwaogopa, tuendelee kulinda heshima na imani tuliyopewa na wananchi” amesema Rais Samia.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments