SERIKALI ya Tanzania imehimiza nchi za Afrika zifanye jitihada kuongeza uzalishaji na tham[1]ani ya zao la kahawa. Rais Samia Suluhu Hassan alisema hayo wakati akifungua mkutano wa nchi zinazozalisha kahawa Afrika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam jana.
Alisema Tanzania imeanza kuipa thamani kahawa yake na kusaidia kutoa ajira kwa vijana kupitia mradi wa Jenga Kesho iliyo Bora (BBT) na iko tayari kufundisha nchi nyingine ili vijana wa Afrika wapate ajira.
“Na sio kahawa tu, BBT inaelekeza pia kilimo cha mazao mengine ya biashara, ufugaji na uvuvi, kwa sasa Tanzania kila zao ni la bi[1]ashara kwa hiyo tupo tayari kufundisha nchi nyingine kama zinahitaji,” alisema Rais Samia.
Aliongeza: “Kwa Tanzania tumepanga mpaka ikifika mwaka 2030, asilimia 20-25 ya kahawa tunayozalisha if[1]anyiwe uchakataji hapa hapa nchini”. Rais Samia alisema kahawa ya Afrika imekuwa ikiuzwa nje, ikiwa ghafi kwa fedha kidogo na kisha inanunuliwa tena kwa fedha nyingi hivyo kusababisha watu wake waendelee kuwa masikini.
“Nikiwa nje hapo (JNICC) nimeona maonesho kwa vijana wetu jinsi kahawa ile ikiwa shamba mpaka inakwenda kuchakatwa, sasa tunakwenda kushindana kwenye uzalishaji na uon[1]gezwaji wa kahawa ndani ya Bara la Afrika,” alisema. Juzi Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alisema Afrika inaingiza dola za Marekani bilioni tatu kwa kuuza ka[1]hawa ghafi lakini inatoa Dola za Marekani bilioni 50 kuin[1]giza kahawa iliyopandishwa thamani.
Rais Samia alisema takwimu zinaonesha kila siku watu wanakunywa vikombe takribani bilioni tatu vya kahawa dunia nzima na kati ya hivyo kahawa nzuri ni ya Afrika lakini kumekuwa na changamoto nyingi. Alisema Afrika imepoteza hadhi yake kwenye sekta ya kahawa duniani hivyo lazima yafanyike marekebisho ku[1]hakikisha furaha ya waku[1]lima wa kahawa inarejea.
“Miaka ya 1960 uzalishaji ilikuwa asilimia 25 lakini sasa uzalishaji umeshuka na kufikia asilimia 11 ya kahawa yote inayozalishwa duniani licha ya soko la kahawa kuwa kubwa duniani, manufaa na fursa tunazopata kulingani[1]sha na nchi nyingine duniani pia yameshuka,” alisema Rais Samia.
Alisema mnyororo wa thamani ya kahawa duni[1]ani unaokadiriwa kufikia thamani ya Dola bilioni 500 Afrika inaambulia asilimia 0.3, zaidi ya asilimia 90 ya mapato yanayopatikana na kahawa inayozalishwa Afrika inakwenda nje. “Wazalishaji ni sisi lakini faida inakwenda kwingine na sisi tunabaki kama shamba tu… inabidi tuitazame vizuri kama Waafrika na tubadilike, changamoto hii ya kimka[1]kati sioni namna inaweza kutatuliwa bila jitihada zetu wenyewe,” alisema Rais Samia.
Kuhusu changamoto ya kibiashara baina ya Afrika, Rais Samia alisema ni lazima Waafrika wasimame vizuri kuuziana wenyewe kwa wenyewe kahawa yao. Alisifu jitihada za kuanzishwa jukwaa la G-25 ambalo limeingiza kahawa kama zao la kimkakati katika Dira ya 2063 ya Umoja wa Afrika.
“Huu ni mwanzo tu, tuna mengi ya kufanya kurudisha hadhi ya kahawa yetu naamini jukwaa hili ni nyenzo sahihi kutufiki[1]sha tunapotaka Kwenda,” alisema Rais Samia. Alishauri Shirikisho la Kahawa Afrika (IACO) kuwa na utaratibu wa kufuatilia maazimio yao, ikiwemo la Dar es Salaam na lile la Uganda. “Na kabla ya kwenda kwenye mkutano ujao wa G-25 2027 Ethiopia tuwe tumeshajua tunakwendaje,” alisema Rais Samia. Alizitaka nchi za Afrika kutazama fursa nyingine ya zao la kahawa kama kuten[1]geneza chai kupitia majani yake, vipodozi, dawa za kuulia wadudu, karatasi na penseli.
“Tukifanya yote hayo ndani ya Afrika tutafanya vizuri, kuendelea kusafirisha kahawa ghafi ni kusafiri[1]sha ajira za vijana wetu na kujikosesha mapato… wema huanzia nyumbani tunaweza kuanza kuuziana kahawa kwenye soko huru la Afrika,” alisema Rais Samia huku akiishauri Burundi kufanya ushirika na Tanzania kwenye kuuza kahawa.
0 Comments