MABINGWA WA MKOA WA SINGIDA WASEMA ASANTE BIOSUSTAIN

                                 

Maandalizi ya kuelekea Ligi ya Mabingwa wa Mikoa nchini, inayotarajiwa kuanza tarehe 13 Machi 2025 katika kituo cha Kigoma, yameanza rasmi kwa Bingwa wa Mkoa wa Singida, timu ya Magic Pressure fc, kuanza kupokea michango mbalimbali kutoka kwa wadau wa soka ndani na nje ya mkoa wa Singida.

Uongozi wa timu hiyo umezungumza na wanahabari wa mkoa wa Singida kwenye ukumbi wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Singida (SIREFA) kuhusu maandalizi yao, huku wakipokea msaada muhimu kutoka kwa Mkurugenzi wa Kiwanda cha Pamba cha Biosustain, Sajad Haider.

                              

Akizungumzia maandalizi hayo, Katibu wa Magic Pressure, Abuu Juma, amesema kuwa timu yao ipo tayari kwa mashindano hayo, kimwili, kiufundi na kiakili, huku wakitambua ushindani mkubwa kwani kila timu inapigania kusonga mbele katika hatua inayofuata.

Kwa upande wake, Sajad Haider, kama mmoja wa wadau wa soka mkoani hapa, ametoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kuichangia timu hiyo ili iweze kushiriki kikamirifu katika mashindano hayo. 

Aidha, Sajad Haidaer ameonyesha dhamira yake ya kusaidia maendeleo ya michezo mkoani singida  kwa kuchangia shilingi milioni moja na nusu kwa timu ya Magic Pressure.

                                     
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Singida, Hamisi Kitila, amepongeza juhudi za Magic Pressure na kueleza kuwa mkoa una dhamira ya kuhakikisha Singida inakuwa na timu zingine zinazoshiriki ligi za madaraja ya chini, mbali na Singida Black Stars, ili kuongeza ushindani na kukuza vipaji vya wachezaji chipukizi mkoani hapa.

                                        

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments