Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo, Machi 21, 2025 amewasili Mkoani Njombe ambapo pamoja na mambo mengine atakuwa Mgeni Rasmi katika kilele cha Siku ya Misitu Duniani inayofanyika kitaifa Mkoani Njombe.
Akiwa Mkoani humo, Mheshimiwa Waziri Mkuu ametembelea kiwanda cha uchakataji mazao ya misitu cha TANWAT (Tanganyika Wattle Company Limited) kilichopo Njombe mjini ambapo ameshuhudia shughuli mbalimbali zinazofanywa na kiwanda hicho.
Akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda hicho Waziri Mkuu amewasihi wafanyakazi wa kiwanda hicho kufanya kazi kwa weledi ili kufanikisha malengo ya muwekezaji.
"fanyeni kazi kwa uaminifu, fanyeni kazi kwa uadilifu, na kwa weledi".
0 Comments