
RC Makonda amesema hayo leo jijini Arusha wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia ‘Samia Legal Aid Campaign’ itakayoendeshwa na timu ya wanasheria kwa siku kumi kwenye halmashauri saba za mkoa huo.
Makonda amesema atashughulika na wakurugenzi watakaoshindwa kutatua changamoto zilizoibuka katika kampeni hiyo na kusisitiza heshima ya Samia legal Aid itunzwe.

“Hatutaki wanaposikilizwa wananchi halafu maagizo yakatolewa atokee kiongozi hataki kutatua mgogoro huo nitakula naye sahani moja,”amesema Makonda.
0 Comments