Taifa Stars yaifuata Morocco kufuzu Kombe la Dunia

TIMU ya Taifa “Taifa Stars” imeondoka leo kuelekea Morocco kwenye mchezo wa Kundi E wa kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya wenyeji Morocco utakaochezwa Machi 26.

Mchezo huo utafanyika kwenye uwanja Uwanja wa Honneur uliopo Manispaa ya d’Oujda.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma alikabidhi bendera ya Taifa kwa wachezaji wa Taifa Stars kabla ya safari hiyo kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro.

Morocco inaongoza kundi E ikiwa na pointi 9 baada mechi 3 ikiwa ikifuatiwa na Niger yenye pointi 6, Tanzania ikiwa ya 3 kwa kukusanya pointi 6, Zambia ikishika nafasi ya 4 kwa pointi 3 baada ya michezo 4 na Congo ipo nafasi ya 5 haina pointi.

Fainali za Kombe la Dunia 2026 zitafanyika kati ya Juni 11 na Julai 19, 2926 zikiandaliwa kwa pamoja na Canada, Mexico na Marekani.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments