DOHA: RAIS wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Felix Tshisekedi, na mwenzake wa Rwanda, Paul Kagame, wamefanya mazungumzo ya ana kwa ana mjini Doha, Qatar, jana. Mazungumzo hayo yalilenga kutafuta suluhu ya mgogoro unaoendelea mashariki mwa DRC.
Viongozi hao walikubaliana kutoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano katika eneo hilo. Taarifa iliyotolewa na Qatar, ambaye alikuwa mpatanishi, imesema usitishwaji huo unapaswa kufanyika bila masharti yoyote.
Hata hivyo, DRC bado inazituhumu Rwanda kwa kuhusika katika kupeleka silaha na majeshi kusaidia wanamgambo wanaoendesha mashambulizi katika eneo la mashariki mwa Congo, ambalo limekumbwa na ghasia kwa miongo kadhaa.
0 Comments