SHINYANGA; MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amewasili mkoani Shinyanga kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu.
Wasira amepokelewa mkoani humo leo Machi 26, 2025 akiwa ameongozana na viongozi mbalimbali wakiwemo baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM.
Ziara hiyo ina lengo la kukagua uhai wa chama, utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025, kusikiliza changamoto za wananchi pamoja na kuhutubia mikutano ya hadhara.
0 Comments