
Mgogoro wa kisiasa watinga wilayani Manyoni baada ya Mkuu wa Wilaya, Dkt. Vincent Mashinji, kumtetea mtendaji wa kata aliyelalamikiwa na wananchi kwa tuhuma za utendaji mbovu.
Katika mkutano uliohudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Bi. Martha Mlata, wananchi walitaka mtendaji huyo aondolewe mara moja, lakini DC akasimama kidete kumlinda, akisisitiza kuwa taratibu za kisheria lazima zifuatwe.
Kauli hiyo imezua mvutano mkali, baadhi ya wanachama wa CCM wakidai uongozi unawapuuza wananchi. Bi. Mlata ametoa kauli ya upatanishi, akiahidi CCM italishughulikia suala hilo kwa haki na weledi.
Na Rafulu Kinala Singida
0 Comments