Tanzania Yazalisha Gesi Asilia Futi Bilioni 301.33 kwa Miaka Minne – PURA

 MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Charles Sangweni amesema kwa kipindi cha miaka minne kuanzia Machi 2021 hadi Machi 2025, kiasi cha gesi asilia kilichozalishwa kimefikia futi za ujazo Bilioni 301.33.

Ameyasema hayo Mei 19, 2025 Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa habari katika kikao kazi kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Amesema kati ya kiasi hicho, futi za ujazo bilioni 142.35 zilizalishwa kutoka Kitalu cha Mnazi Bay na futi za ujazo bilioni 158.98 kutoka Kitalu cha Songo Songo.

"Uzalishaji huu ni wastani wa futi za ujazo Bilioni 35.59 kwa mwaka kwa upande wa Mnazi Bay na futi za ujazo Bilioni 39.74 kwa mwaka kwa upande wa Songo Songo". Amesema

Aidha Sangweni amesema kuwa kwa kipindi cha nyuma, uzalishaji wa gesi ulikuwa wastani wa futi za ujazo Bilioni 32.03 kwa mwaka kwa upande wa Mnazi Bay na futi za ujazo Bilioni 25.13 kwa mwaka kwa upande wa Songo Songo.

Amesema Gesi asilia iliyozalishwa ilitumika kwa matumizi mbalimbali ikiwemo uzalishaji wa umeme; matumizi ya viwandani, majumbani, taasisi, na katika magari.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments