Washiriki wakiwa katika jukwaa la 'Kijiwe cha Kahawa' lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa ajili ya kujadili Bajeti ya Taifa kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kwa mtazamo wa kijinsia, wakifuatilia mubashara Hotuba ya Hali ya Uchumi iliyowasilishwa Bungeni Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wadau kutoka sekta mbalimbali nchini wamekutana katika jukwaa la 'Kijiwe cha Kahawa' lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa ajili ya kujadili Bajeti ya Taifa kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kwa mtazamo wa kijinsia.
Tukio hilo muhimu linafanyika katika ofisi za TGNP, ambapo limewaleta pamoja wanachama wa mtandao huo, wakurugenzi wa bodi, wanazuoni, wawakilishi kutoka taasisi za umma, asasi za kiraia, sekta binafsi, wanahabari, pamoja na wanachama kutoka mikoa mbalimbali.
Akizungumza wakati wa kufungua mjadala huo, Kaimu Mkurugenzi wa TGNP, Clara Kalanga, ambaye ni Mkuu wa Programu - TGNP, Clara Kalanga amesema mjadala huo una lengo la kuchochea mabadiliko chanya ya kisera na kiutendaji kupitia uchambuzi wa bajeti ya taifa kwa jicho la kijinsia.
Amewataka washiriki kuendeleza mazungumzo na kutoa mapendekezo ya kuboresha utekelezaji wa bajeti ya mwaka huu kwa maslahi ya wote.
“Tunakutana hapa siyo tu kwa ajili ya kufuatilia bajeti, bali pia kutathmini utekelezaji wake kwa kuzingatia changamoto za makundi yaliyopo pembezoni – wanawake, vijana, watu wenye ulemavu na wanaume maskini,” amesema Kalanga.
Katika mjadala huo, washiriki wamepata fursa ya kufuatilia mubashara Hotuba ya Hali ya Uchumi iliyowasilishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, pamoja na Hotuba ya Bajeti ya Taifa itakayowasilishwa bungeni na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba.
TGNP imesema kuwa kupitia jukwaa la ‘Kijiwe cha Kahawa’ ambalo limekuwepo tangu mwaka 2016, wameendelea kujenga ushirikiano na wadau mbalimbali katika kuhakikisha sauti za wananchi, hususan makundi ya pembezoni, zinazingatiwa katika upangaji wa bajeti ya taifa.
Katika mjadala wa mwaka huu, dhima kuu ni: “Ujenzi wa Jamii yenye Usawa, Uzingatiaji wa Bajeti Yenye Mrengo wa Kijinsia kuelekea Bajeti ya Taifa 2025/26 na Uwekezaji kwenye Usawa wa Kijinsia, Haki za Wanawake na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.”
TGNP imesisitiza kuwa maarifa yanayotokana na mjadala huu yataendelea kutumika kama nyenzo muhimu kwa ajili ya kuhamasisha ushiriki mpana na kufuatilia utekelezaji wa bajeti kwa mlengo wa kijinsia ili kuhakikisha rasilimali za taifa zinawanufaisha wote kwa usawa.
Kwa miaka 32 sasa, TGNP imekuwa ikitekeleza mchakato wa ufuatiliaji wa bajeti kwa kushirikiana na wananchi kupitia mbinu ya Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O&OD) ili kuhakikisha vipaumbele vya jamii vinafikishwa hadi katika ngazi ya kitaifa.
Kaimu Mkurugenzi wa TGNP, Clara Kalanga, ambaye ni Mkuu wa Programu - TGNP, Clara Kalanga akifungua Mjadala katika jukwaa la 'Kijiwe cha Kahawa' lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa ajili ya kujadili Bajeti ya Taifa kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kwa mtazamo wa kijinsia uliofanyika katika ukumbi wa TGNP Jijini Dar es salaam
Kaimu Mkurugenzi wa TGNP, Clara Kalanga, ambaye ni Mkuu wa Programu - TGNP, Clara Kalanga akifungua Mjadala katika jukwaa la 'Kijiwe cha Kahawa' lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa ajili ya kujadili Bajeti ya Taifa kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kwa mtazamo wa kijinsia uliofanyika katika ukumbi wa TGNP Jijini Dar es salaam
Washiriki wakiwa katika jukwaa la 'Kijiwe cha Kahawa' lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa ajili ya kujadili Bajeti ya Taifa kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kwa mtazamo wa kijinsia, wakifuatilia mubashara Hotuba ya Hali ya Uchumi iliyowasilishwa Bungeni Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo.
Washiriki wakiwa katika jukwaa la 'Kijiwe cha Kahawa' lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa ajili ya kujadili Bajeti ya Taifa kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kwa mtazamo wa kijinsia,wakifuatilia mubashara Hotuba ya Hali ya Uchumi iliyowasilishwa Bungeni Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo.

0 Comments