Diwani Kinyeto Atoa Milioni 2.6 kwa Michezo na Ulinzi wa Kura Kata ya Kindai

Katika kuendeleza juhudi za kuimarisha michezo na usalama wa demokrasia ngazi ya jamii, Diwani wa Kata ya Kindai, Mhe. Omary Salum Kinyeto, ametumia jumla ya shilingi milioni 2.6 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya michezo na kombati za vikundi vya ulinzi maarufu kama Green Guard.

Vifaa hivyo vimekabidhiwa kwa timu mbalimbali za mpira wa miguu za kata hiyo ili kuhamasisha ushiriki wa vijana katika michezo, huku kombati zikikabidhiwa kwa vikundi maalum vitakavyohusika na kulinda usalama wa kura na mazingira katika kipindi cha uchaguzi kijacho.

Mhe. Kinyeto amesema kuwa hatua hiyo inalenga kuwajengea vijana moyo wa uzalendo, ushirikiano, na kuwapa nafasi ya kushiriki katika maendeleo ya kijamii na kisiasa.

“Tumetumia shilingi milioni 2.6 kwa ajili ya kuinua vipaji kupitia michezo na kuandaa vijana watakaosaidia kulinda haki ya kidemokrasia wakati wa uchaguzi. Huu ni uwekezaji kwa maendeleo ya Kindai,” alisema Mhe. Kinyeto.

Aidha, Diwani huyo ametangaza kuwa mashindano ya Kindai Cup yataanza hivi karibuni, yakihusisha timu kutoka mitaa yote ya kata hiyo. Mashindano hayo yanatarajiwa kuwa chachu ya mshikamano na uhamasishaji wa amani kipindi cha uchaguzi.

Wakazi wa Kata ya Kindai wamepokea hatua hiyo kwa furaha, wakieleza kuwa ni uthibitisho wa uongozi unaowajali watu na kuwekeza kwa vitendo katika maendeleo ya jamii.


Na  Abdul Ramadhani Singida

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments