Diwani Omary Kinyeto Aanza Rasmi Ziara ya Ilani, Atoa Mlango Mpya kwa Ofisi ya Mtaa Mahembe

                                       

Diwani wa Kata ya Kindai, Mheshimiwa Omary Salum Kinyeto, leo ameanza rasmi ziara yake ya kuwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama kwa kipindi cha mwaka 2020 hadi 2025, kwa kufanya mkutano wake wa kwanza wa hadhara katika Mtaa wa Mahembe kati ya mikutano saba inayotarajiwa kufanyika katika kata hiyo.

Katika mkutano huo, Diwani Kinyeto alitoa taarifa ya mafanikio mbalimbali yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitano, ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kama ujenzi wa shule, barabara, ofisi za serikali za mitaa, upandaji miti, na uwezeshaji wa vikundi vya ujasiriamali kwa vijana na wanawake.

Katika hatua iliyowagusa wengi, Mheshimiwa Diwani alikabidhi mlango mpya kwa Ofisi ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Mahembe, kufuatia kuibiwa kwa mlango wa awali. Tukio hilo liliibua shangwe na pongezi kutoka kwa wananchi waliokuwepo, kama ishara ya uongozi wa karibu na unaojali ustawi wa jamii.

“Mikutano hii inalenga kuwahabarisha wananchi kile tulichotekeleza, kusikiliza changamoto zao na kuandaa mikakati ya pamoja ya maendeleo ya baadaye,” alisema Mh. Kinyeto katika hotuba yake.

Wananchi wa Mahembe walionesha kuridhika na hatua mbalimbali za maendeleo zilizotekelezwa katika kata yao huku wakitoa maoni na mapendekezo ya maeneo yanayohitaji kipaumbele zaidi.

Ziara hiyo inaendelea katika mitaa mingine ya Kata ya Kindai, ikiwa ni sehemu ya uwazi na uwajibikaji wa uongozi wa kata kwa wananchi wake.

Picha mbali mbali katika mkutano huo

Singida – Kata ya Kindai: Abdul Ramadhani

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments