KULWA BITEKO ACHUKUA FOMU UBUNGE JIMBO LA KATORO

 Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kulwa Biteko kwa mara nyingine amechukua fomu ya kugombea ubunge katika Jimbo jipya la Katoro lililopo katika mamlaka ya mji mdogo wa Katoro wilayani Geita.

Hii ikiwa ni muendelezo wa harakati zake kisiasa,ambapo mnamo mwaka 2020 alichukua fomu ya kugombea jimbo hilo ambalo hapo kabla liliitwa jimbo la Busanda.

Jimbo la katoro lilipatikana baada ya mchakato wa kugawa majimbo ulipokamilika na kupata majimbo mawili yaani jimbo la Katoro na Jimbo la Busanda.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Geita Michael Msuya amesema kuwa dirisha la uchukuaji wa fomu za ubunge na udiwani limefunguliwa rasmi leo tarehe 28 kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa 10 jioni.

Amewasihi watia nia kufata kanuni za chama kutoleta mbwembwe wakati wa uchukuaji wa fomu hizo ili kuondoa vurugu ambazo hazina msingi.





TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments