NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi,akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 12,2025 jijini Dodoma katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga Utumikishwaji wa Watoto.
Na.Alex Sonna-DODOMA
NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi amesema takwimu zinaonesha kuwa utumikishaji wa Watoto umepungua kutoka asilimia 29 mwaka 2014 hadi asilimia 24.9 mwaka 2021 kwa mujibu wa Utafiti Jumuishi wa Nguvu Kazi.
Licha ya mafanikio hayo, imepanga kufanya ukaguzi maalum kwa wiki mbili kwenye maeneo mbalimbali ili kuwabaini na kuwachukulia hatua wanaotumikisha watoto.
Akizungumza jijini Dodoma katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga Utumikishwaji wa Watoto, Naibu Waziri Katambi, amesema ukaguzi huo utafanyika kwenye hasa ya migodi, mashamba, viwanda na maeneo mengine yote ambayo kazi zinafanyika.
Hata hivyo, amesema serikali imeanzisha mikakati mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mpango Kazi wa Taifa wa Kupinga Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWA II, 2024/25–2028/29) na Mkakati wa Taifa wa Kutokomeza Utumikishwaji wa Watoto, ambao unalenga kuunganisha nguvu za wadau wote wa maendeleo, mashirika ya kiraia na jamii kwa ujumla.
“Ni marufuku kutumikisha watoto, nitoe wito kwa waajiri wote nchini kuhakikisha hawajihusishi na ajira za watoto. Kaguzi zinaendelea kufanyika na wale watakaobainika, sheria itachukua mkondo wake bila ajizi,” ameonya Katambi.
Amesisitiza serikali itaendelea kutoa elimu kwa umma, kushirikiana na wadau, na kuhakikisha utekelezaji wa sheria kama Sheria ya Mtoto Sura ya 13 na Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini, Sura 366 unafanyika kwa ukamilifu.
Naye, Mratibu wa miradi kitaifa wa Shirika la Kazi Duniani (ILO), Glory Blasio, amepongeza Tanzania kwa hatua kubwa ya kukabiliana na utumikishaji huo huku akidai kwa kiasi kikubwa utumikishaji bado upo kwa watoto wa kike.
Kamishna wa Kazi, Suzan Mkangwa, amesema katika kuadhimisha siku hiyo watafanya kaguzi na kutoa elimu kwa wazazi kujiepusha na utumikishaji watoto kwa kuwa unakiuka sheria na miongozo ya nchi.

0 Comments