Katika miji mingi ya Tanzania, kazi ya kuokota taka imekuwa njia muhimu ya kuilinda mazingira na kusaidia usafi wa miji,Vijana na wanawake wengi wanajihusisha na kazi hii kwa bidii, lakini mara nyingi hawapati elimu wala msaada wa kifedha unaowasaidia kuimarisha maisha yao,Changamoto hii imekuwa kikwazo kikubwa kwao kujiletea maendeleo ya kudumu.
Hili limebadilika kupitia mpango wa kipekee wa Benki ya Equity, ambao kwa kushirikiana na taasisi ya JUZA Waste Pickers Initiative na Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira, limeanzisha semina za kutoa elimu ya fedha kwa waokota taka,Lengo ikiwa ni kuwajengea uwezo wa kuwekeza, kuweka akiba na kupanga matumizi yao vizuri ili kazi wanayofanya isitoe tu kipato cha haraka, bali iwe njia ya maendeleo ya kweli kwao binafsi na familia zao.Balozi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira , Grit Mwimanzi ( kulia ) akifurahia jambo na Kaimu Meneja wa NEMC Kanda ya Ilala Bi. Abela Murungi ( kushoto ) muda mfupi baada ya Hotuba yake.
Balozi wa Mazingira, Grit Mwimanzi, amesema mpango huu ni hatua muhimu katika kutambua mchango wa waokota taka katika uchumi wa kijani na kuhakikisha wanapata fursa sawa na wafanyakazi wengine katika sekta nyingine,Pia, anasisitiza kuwa elimu ya fedha ni nyenzo muhimu ya kuwasaidia kujiletea maendeleo binafsi na kuchangia ustawi wa taifa kwa ujumla.
Naye Meneja wa Kitengo cha Wanawake na Vijana wa Benki ya Equity, Jackline Temu, ameeleza kuwa kupitia dirisha la Mwanamke Plus, benki imetambua kuwa wengi wa wanawake na vijana wanaojihusisha na uokotaji taka wana kipato kinachoweza kuongezeka zaidi kama wangekuwa na maarifa ya kifedha,Kupitia semina hizo, wamefunguliwa akaunti za benki na kupewa elimu ya kuweka akiba na kupanga matumizi, hatua inayowawezesha kujiletea maendeleo endelevu.Kwa upande wao, wadau wa mazingira kama taasisi ya JUZA Waste Pickers Initiative na Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wanahamasisha jamii kubadili mtazamo wa kuwaona waokota taka kama watunzi wa mazingira na washiriki muhimu wa uchumi wa kijani wanasisitiza kuwa kuwapatia elimu ya kifedha ni njia mojawapo ya kuwainua kiuchumi na kuhakikisha kazi yao inaendelea kwa mafanikio na heshima.Kwa kuleta elimu ya fedha kwa kundi hili ambalo kwa muda mrefu limekuwa likikumbwa na changamoto mbalimbali, Benki ya Equity na wadau wake wanasaidia kuweka msingi imara wa maisha bora, maendeleo endelevu, na mazingira safi kwa kizazi cha sasa na kijacho.
0 Comments