Kura hizo za maoni zilizofanyika Julai 30, 2025, zimewaweka wawili hao kileleni kwa kuibuka kidedea dhidi ya wagombea wenzao waliowania nafasi hizo ndani ya CCM. Ushindi huu umetafsiriwa kama ishara ya kuaminiwa kwao na wajumbe kutokana na mchango wao ndani ya chama na jamii kwa ujumla.
Wachambuzi wa siasa mkoani humo wanasema ushindi huu sio wa bahati, bali ni matokeo ya uaminifu, uadilifu na juhudi walizoweka katika kutetea maslahi ya wanawake na jamii ya Singida kwa ujumla.
Wanachama na wafuasi wa CCM wamefurika mitandaoni kuwapongeza viongozi hao huku wakieleza matumaini yao kuwa wataendelea kusimamia ipasavyo maendeleo ya wanawake na vijana mkoani humo.
"Hawa ni wanawake wa kazi! Ushindi wao umetokana na ukweli kwamba hawakuwahi kuwasaliti wananchi wala chama," alisema mmoja wa wanachama waliohojiwa.
Mchakato wa kura za maoni unaendelea kushika kasi mikoa mbalnaimbali nchini huku CCM ikijiandaa na uchaguzi mkuu ujao.


0 Comments