Singida Yasimama Pamoja Moto Wazimwa Soko Kuu Kwa Juhudi Za Pamoja

Katika hali ya taharuki iliyotokea mapema leo, moto ulizuka katika Soko Kuu la Manispaa ya Singida, ukiteketeza baadhi ya vibanda na bidhaa kabla ya kudhibitiwa na Kikosi cha Zimamoto kwa ushirikiano na wananchi.

Tukio hilo limeibua hisia na mshtuko kwa wakazi wa Singida, ambapo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Bi. Martha Mlata, alitembelea eneo la tukio na kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaleta viongozi makini katika mkoa huo.

                                     

Bi. Mlata amempongeza Mkuu wa Mkoa Bi. Halima Dendego pamoja na timu yake kwa kuchukua hatua za haraka katika kushughulikia tukio hilo na kuwa bega kwa bega na wananchi wakati wa janga hilo.

"Tunaiona kazi ya viongozi wetu, wamekuwa wa haraka, wa makini, na wanawajali wananchi. Hii ndiyo maana tunampongeza sana Rais wetu kwa kutupelekea watendaji wa namna hii," alisema Bi. Mlata mbele ya wananchi waliokusanyika katika soko hilo.

Moto huo umezimwa kwa juhudi za pamoja, na mamlaka husika zinaendelea kuchunguza chanzo cha tukio hilo ili kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa.

Abdul Ramadhani Singida.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments