“Uongozi Wenye Matendo, Si Maneno – Kingu na Mgonto Ndiyo Jibu”

Siasa za Wilaya ya Ikungi zimepamba moto baada ya wabunge wawili wanaopendwa na kuthaminiwa, Mhe. Elibariki Kingu (Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi) na Mhe. Thomas Mgonto (Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki), kurejesha rasmi fomu za kuomba ridhaa ya wananchi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuendelea kulitumikia taifa.

Mapokezi yao yaligeuka kuwa sherehe ya amani, mshikamano na matumaini, huku maelfu ya wananchi wakiimba nyimbo za hamasa na kubeba mabango ya kuonesha imani yao kwa viongozi hao wawili.

Mhe. Kingu na Mhe. Mgonto wameendelea kutambulika kama nguzo muhimu za maendeleo katika Ikungi, wakijipambanua kwa kutekeleza miradi mikubwa ya kijamii ikiwemo uboreshaji wa elimu, huduma za afya, miundombinu ya barabara, maji safi na kuendeleza vijana kupitia ajira na michezo.

                                  

Kwa sauti moja, wananchi wa Ikungi wameahidi kuendelea kuwaunga mkono viongozi wao waaminifu na wachapa kazi, wakisisitiza kuwa Kingu na Mgonto ndiyo tumaini la kupeleka Ikungi mbele zaidi katika maendeleo endelevu.

Abdul Ramadhani -Singida 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments