Pinda ataka Matokeo ya Utafiti yazingatiwe kueleza faida za Kisanyansi katika bidhaa za Kilimo

Waziri Mkuu mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Pinda ametaka Utaalamu wa Kisanyansi uzingatiwe katika mnyororo mzima wa thamani wa sekta ya Kilimo ikiwa ni pamoja na kuzingatia ufafanuzi wa Kisanyansi katika chapa za bidhaa mbalimbali za Kilimo zilizoongezewa thamani ili kuonesha tija inayopatikana kwa mtumiaji wa bidhaa hizo.

Mheshimiwa Pinda amesema hayo Leo Agosti 07,2025 alipokuwa katika Banda la Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) kwenye Maonesho ya kimataifa ya Kilimo Maarufu kama Nanenane yanayoendelea viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma ambapo TARI inashiriki ikiwa na Teknolojia mbalimbali za Kilimo.

Akitolea mfano wa Korosho iliyoongezewa thamani na TARI Mheshimiwa Pinda ameeleza kufuraishwa na ufafanuzi wa kitaalamu uliopo katika mfuko wa Korosho hizo unaotoa maelezo ya Kisanyansi kumtosheleza mtumiaji kutambua tija anayopata kutokana na matumizi ya bidhaa hiyo zaidi ya kuishia kusema ni tamu yenye ladha nzuri kitu ambacho amesema kinanyima fursa zaidi kwa mtumiaji kuelewa.

Akiwa katika Banda la TARI, Waziri Mkuu huyo mstaafu amepata maelezo kuhusu Teknolojia mbalimbali za Kilimo zilizofanyiwa Utafiti na TARI ambazo amewasihi wadau wa Kilimo kuzitumia ili kujiongezea tija.



TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments