Waandishi wa Habari Singida Wapandishwa Vilele vya Uelewa wa Usalama kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

                                          

Ukumbi wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Singida   umefurika bashasha na mijadala ya kina, huku waandishi wa habari  kujifunza mbinu za kujilinda kimwili, kidijitali na kisaikolojia katika mazingira yao ya kazi.

Mafunzo hayo, ambayo yamekuja katika kipindi nyeti kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, yameendeshwa na mkufunzi  Jamalidini Abuu,  Akizungumza kwa msisitizo, Jamalidini Abuu aliwakumbusha wanahabari kuwa usalama wao ni msingi wa kazi bora.

"Ulinzi wa mwandishi huanzia kwake mwenyewe. Simameni kama walinzi wa taarifa zenu na ustawi wenu. Hata kamera yenye thamani kubwa haina maana kama usalama wako uko mashakani," alisema huku akipigiwa makofi na washiriki.

                                      

Aliwahimiza waandishi kuhakikisha vifaa vyao vya kazi vinalindwa ipasavyo, kutumia nywila imara, kuepuka viunganishi visivyo salama na kuweka uthibitishaji wa hatua mbili (Two-Factor Authentication) ili kuimarisha usalama wa taarifa.

Bw. Amini Nyaungo, mmoja wa washiriki, alisema mafunzo hayo yamemfungua macho zaidi kuhusu namna anavyoweza kujilinda katika kazi.

"Kabla ya mafunzo haya nilikuwa sitilii mkazo sana masuala ya usalama wa kidijitali, sasa najua thamani yake. Nitayatekeleza mara moja," alisema kwa furaha.

                                         

Mafunzo haya ni sehemu ya mradi wa “Empowering Journalists for Informed Community” unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) na Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC), ukitekelezwa na International Media Support (IMS)Union of Tanzania Press Clubs (UTPC) na JamiiAfrica.

                                      

Mbali na elimu ya usalama wa kimwili na kidijitali, washiriki pia walijifunza mbinu za kulinda afya ya akili ili kuhimili changamoto za kitaaluma na maisha binafsi.

Kwa mujibu wa Jamalidini Abuu, mafunzo haya yamekusudia kuandaa wanahabari kuwa mstari wa mbele katika kuripoti matukio kwa usahihi bila kuhatarisha maisha yao, hasa katika kipindi chenye msisimko wa kisiasa.

Na Alifu Abdul

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments