Yagi Kiaratu Aendelea Kunga’ara Singida Mjini – Historia Ya Uongozi Imara Yampa Heshima

Yagi Kiaratu, mmoja wa viongozi wanaoaminiwa na kuheshimika katika Manispaa ya Singida, ameendelea kuwa gumzo baada ya kuonyesha nia thabiti ya kuendelea kulitumikia jimbo la Singida Mjini. 
Kiaratu, ambaye alishawahi kuhudumu kama Meya wa Manispaa ya Singida, anasifika kwa uongozi wake ulioweka msingi wa miradi mingi ya maendeleo, ikiwemo miundombinu, huduma za jamii, na kusimamia ushirikishwaji wa wananchi katika maendeleo.

Kwa wengi, Yagi si tu kiongozi bali ni mfano wa uwajibikaji, unyenyekevu, na mtu wa watu. Ndani ya nyanja za siasa na jamii, jina lake linaendelea kung’ara kutokana na utendaji wake uliojikita kwenye matokeo na uwazi kwa wananchi.

Wananchi wa Singida Mjini sasa wana kila sababu ya kuwa na matumaini mapya, kwani Kiaratu amerudi na dira mpya, akiwa amejaa uzoefu, maono na ari ya kuendelea kuijenga Singida ya kisasa, yenye fursa kwa watu wote.

“Uongozi ni dhamana. Tunapopewa nafasi hatupaswi kuhutubia watu kwa maneno matupu, bali kwa vitendo vyenye tija. Ndiyo falsafa yangu,” alinukuliwa Kiaratu akisema wakati wa mahojiano ya hivi karibuni.

Wananchi sasa wana nafasi ya kuchagua mtu mwenye historia ya utendaji, mtu anayewajua, na mtu aliyewahi kuwa sehemu ya mafanikio ya kweli ya Singida 
Na Abdul Ramadhani Singida

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560

Post a Comment

0 Comments