Yagi Kiaratu – Kiongozi Anayejali Maslahi ya Wananchi Singida Mjini

                               

Yagi Kiaratu, Mbunge alieteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea Ubunge wa Jimbo la Singida Mjini kupitia michakato ya ndani ya chama, ameendelea kuthibitisha kuwa kiongozi anayejali na kuthamini maslahi mapana ya wananchi.

Kiaratu, ambaye aliwahi kuhudumu kama Meya wa Manispaa ya Singida na pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka la Wanawake Mkoa wa Singida, amekuwa akiheshimika kutokana na uadilifu, ukaribu na uelewa wa changamoto za wananchi.

Akizungumza mara baada ya kuteuliwa, Yagi amesema anafikika na yupo tayari kupokea ushauri kutoka kwa wananchi wote kwa maslahi ya jamii na taifa kwa ujumla. Ameahidi kuendeleza mshikamano, mshauri wa maendeleo na mshiriki wa kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa Singida Mjini.

Kwa historia yake ya uongozi, wananchi wengi wameonesha imani kubwa kuwa atakuwa kiungo imara kati ya chama na wananchi, akihakikisha maendeleo yanazidi kupatikana kwa kila mmoja.

Abdul Ramadhani Singida

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments