DK. NCHIMBI APAA KWA HELIKOPTA KUSAKA KURA ZA CCM KAGERA

 MGOMBEA Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, leo Septemba 7, 2025, ameruka kwa helikopta akizisaka kura za kishindo za CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Balozi Dk. Nchimbi ameanza ziara yake ya kampeni Mkoani Kagera kwa kishindo, ambapo atafanya mikutano katika maeneo ya Ngara, Kyerwa, Katoro-Bukoba Vijijini na kuhitimisha kwa mkutano mkubwa Bukoba Mjini.

Katika mikutano hiyo, Dk. Nchimbi atanadi sera na Ilani ya CCM, akieleza mikakati na mipango ya chama hicho endapo kitapewa ridhaa ya kuongoza kwa miaka mitano ijayo.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments