Hali hiyo imebadilika nchini Tanzania kupitia msimamo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally, usawa wa wanaume na wanawake si suala la hiari ndani ya chama hicho, bali ni msimamo wa kifalsafa na kiitikadi unaotekelezwa kwa lazima na vitendo.
Akizungumza leo tarehe 9 Septemba 2025 katika uwanja wa Bombadia, Singida Mjini, mbele ya maelfu ya wananchi waliojitokeza kumlaki na kumsikiliza Mgombea wa Urais kupitia CCM, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Dkt. Bashiru alisema:
“Katika uongozi wa Rais Dkt. Samia, takwimu zinaonesha wazi namna maamuzi, sera na miradi mbalimbali ilivyowawezesha wanawake kujiamini, kushiriki maendeleo na kuinua hali zao kimaisha.”
Alibainisha kuwa mageuzi haya si matokeo ya upendeleo, bali ni jitihada za Rais Samia kuimarisha uwezo wa wanawake kushiriki siasa, uchumi na uongozi kwa ujasiri na ufanisi.
Mwanamke Tanzania Leo
Dkt. Bashiru aliendelea kueleza kuwa, tofauti na miaka ya nyuma ambapo mwanamke alihesabiwa kama msaidizi, leo Tanzania imeweka historia mpya. Mwanamke ameketi kwenye meza moja na mwanaume katika maamuzi makubwa ya kitaifa, kuanzia ngazi za serikali za mitaa hadi baraza la mawaziri.
“Rais Samia hajawapendelea wanawake. Amejenga mfumo wa kuwawezesha kwa vitendo kupitia miradi ya kiuchumi, sera za kijamii na maamuzi ya kisera yenye tija. Matokeo yake ni kizazi cha wanawake jasiri na wenye kujiamini,” alisema.
Samia na Ajenda ya Usawa
Katika kipindi cha miaka yake minne ya uongozi, Rais Samia ameongoza mageuzi ya kimaendeleo yaliyogusa moja kwa moja maisha ya wanawake kupitia:
-
Mikopo ya wanawake kupitia Halmashauri nchini,
-
Programu za ujasiriamali na uwezeshaji kiuchumi,
-
Ushiriki wa wanawake katika siasa kwa uwiano mkubwa zaidi,
-
Uwekezaji katika elimu ya mtoto wa kike na afya ya mama na mtoto.
Kwa mtazamo wa Dkt. Bashiru, haya ni mashahidi hai kwamba Tanzania ya leo imepiga hatua kubwa katika kujenga taifa lenye usawa wa kijinsia.
Hitimisho
Hotuba ya Dkt. Bashiru Singida Mjini imeacha ujumbe wa kina kwa wananchi: kwamba uongozi wa Rais Samia si hadithi, bali ni historia ya vitendo vya usawa, mshikamano na maendeleo jumuishi.
Kwa mara nyingine, Singida Mjini imethibitisha kuwa iko tayari kuunga mkono falsafa ya maendeleo yenye usawa inayosimamiwa na Rais Samia Suluhu Hassan kupitia CCM.
N Mwandishi Wetu Singida.

0 Comments