Kanda ya Kati Yaamka – UWT Watinga Singida kwa Nguvu Mpya



Baada ya mafanikio makubwa katika ziara za Iringa na Dodoma, hatimaye tarehe 30 Septemba ilikuwa ni zamu ya mkoa wa Singida kuunganishwa katika mwamko mpya wa kisiasa unaoongozwa na Waratibu wa Uchaguzi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Kanda ya Kati. Ziara hii muhimu ilianza rasmi wilayani Iramba na kuendelea Singida mjini, ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Waratibu hao, Diana Chilolo.

Mapokezi ya Chilolo na timu yake yamekuwa ya kishindo, yakipokelewa kwa furaha, nderemo na mshikamano wa kipekee kutoka kwa wanawake, vijana na wazee wa CCM. Akihutubia maelfu ya wanachama wa UWT Singida mjini, Chilolo alisisitiza kuwa mshindi wa mwanamke mmoja ni mshindi wa wote.

“Mwanamke mmoja akisimama, anasimama kwa niaba ya wanawake wote. Na mama yetu Samia Suluhu Hassan ana moyo wa kipekee wa kutupa dira na matumaini mapya. Ndiyo maana tunapaswa kusimama imara na kuzisaka kura za wagombea wa CCM usiku na mchana,” alisema Chilolo kwa msisitizo.

Kauli hiyo imeamsha ari na hamasa kubwa miongoni mwa wanachama, huku ikithibitisha dhamira ya UWT kuendelea kusimama mstari wa mbele kulinda na kuimarisha ushindi wa CCM katika uchaguzi wa 2025.

Ziara hiyo sasa inatarajiwa kuendelea katika wilaya zote za mkoa wa Singida, ikibeba ujumbe wa mshikamo, mshindi tayari na mshikikano wa chama tawala kuelekea uchaguzi mkuu.


                             

Alifu Abdul Singida

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments