Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Singida, Bertha Nakomolwa, ameendelea na harakati za kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaibuka na ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu ujao.
Leo ilikuwa ni zamu ya wananchi wa Wilaya ya Ikungi, Kata ya Ingelason, Kitongoji cha Nkurusi, ambapo Nakomolwa aliongozana na viongozi wenzake akiwemo Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi.
Wakiwa na moyo wa kujitoa, walipita kaya kwa kaya na hata saluni za wajasiriamali wadogo, wakizungumza na wananchi kwa ukaribu mkubwa. Katika mazungumzo yao waliendelea kueleza kwa vitendo namna Ilani ya CCM 2020–2025 inavyotekelezwa na kuwaletea maendeleo wananchi kwa masilahi mapana ya Taifa.
Mama Nakomolwa aliwaomba wananchi wote waendelee kuiamini CCM na kuipa kura za NDIYO kwa wagombea wake wote, akisisitiza kuwa chama hiki ndicho chenye historia, sera na vitendo vinavyoakisi maendeleo ya kweli ya Watanzania.
“CCM imeahidi, CCM imetekeleza, na CCM itaendelea kufanya kazi kwa masilahi ya wananchi wote bila kujali dini, kabila wala hali ya kiuchumi,” alisema.
Alifu Abdul Singida

0 Comments