Martha Mlata: “CCM Ni Chaguo la Maendeleo” – Awaongoza Wananchi wa Iramba Mashariki Kumpigia Kura Dkt. Samia, Jesca Kishoa na Madiwani

                                   

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Martha Mlata, ameendelea kuonesha weledi na uhodari wa kisiasa kwa kuhimiza wananchi wa Mkoa wa Singida na maeneo ya jirani kuendelea kuiamini CCM kama nguzo kuu ya maendeleo ya taifa.

Leo, akiwa mgeni rasmi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Gumanga, Wilaya ya Mkalama, Jimbo la Iramba Mashariki, Mlata aliongoza maelfu ya wananchi waliokusanyika kumuunga mkono mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, mgombea ubunge Jesca Kishoa pamoja na madiwani wa CCM.

Katika hotuba yake yenye msisimko, Mlata aliwaasa wananchi kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi tarehe 29 Oktoba kutimiza haki yao ya kikatiba kwa kuwapigia kura wagombea wa CCM. Alisisitiza kuwa CCM imejipambanua kama chama cha ushindi, kinachojali maendeleo ya wananchi na masilahi mapana ya taifa.

                            

“Tunapomchagua Dkt. Samia, tunachagua mshikamano wa taifa, tunachagua maendeleo endelevu na tunachagua kiongozi mwenye dira na maono. Tunapomchagua CCM, tunachagua chama kinachoamini katika mshikamano wa Watanzania wote bila kujali tofauti zao.” – Martha Mlata

Aidha, alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi wa Iramba Mashariki kuhakikisha wanampa kura za kishindo Jesca Kishoa kwa nafasi ya Ubunge, pamoja na madiwani wa CCM katika kata zote, ili kuhakikisha chama kinapata nguvu ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi kwa ufanisi zaidi.

Kwa upande wao, wananchi waliohudhuria mkutano huo walionesha hamasa kubwa kwa kushangilia na kuahidi kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura, wakisisitiza kwamba CCM imeendelea kuwa tegemeo la maendeleo katika jamii.

                       

Kwa ujumla, ziara ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Martha Mlata, inazidi kuimarisha kampeni za chama hicho katika mkoa mzima na kuonesha wazi kuwa umoja wa wananchi na mshikamano wa chama ndio msingi wa ushindi wa kishindo ifikapo tarehe 29 Oktoba.

Alifu Abdul Singida Mkalama

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments