Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Azindua Kampeni Iramba Magharibi

                                   

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Martha Mlata, amewaomba wananchi wa Mkoa wa Singida na Watanzania kwa ujumla kuendelea kuchagua viongozi ambao kipaumbele chao ni kulinda na kuendeleza amani ya nchi pamoja na masilahi ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Ametoa wito huo wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi katika Jimbo la Iramba Magharibi, ambapo aliongoza mkutano wa hadhara iliyohudhuriwa na maelfu ya wananchi.

Katika hotuba yake, Bi. Mlata aliwaomba wananchi kuendelea kuwa imara katika mshikamanon na umoja, huku akihimiza mshikamano katika kulinda amani na maendeleo yaliyopatikana chini ya uongozi wa CCM.

“Tunapaswa kuendeleza amani tuliyo nayo kwa kuchagua viongozi wenye dira na maono ya taifa, viongozi wanaojali wananchi na masilahi ya taifa letu. Amani ndiyo msingi wa maendeleo,” alisema.
Aidha, alitumia nafasi hiyo kuwaombea kura wagombea wa CCM akianzia na mgombea urais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akimwelezea kama kiongozi jasiri na mwenye dhamira ya kweli ya kuwaletea maendeleo Watanzania wote.

Vilevile alimuombea kura Dkt. Mwigulu Nchemba, mgombea ubunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, na wagombea wote wa nafasi za udiwani katika kata mbalimbali za jimbo hilo.

Bi. Mlata alibainisha namna ambavyo Ilani ya CCM imetekelezwa kwa mafanikio makubwa katika kipindi kilichopita, na akawahakikishia wananchi kuwa utekelezaji zaidi utafanyika kwa kasi kubwa zaidi katika awamu inayofuata.

Amewakumbusha wananchi kuendelea kutunza vitambulisho vya kupiga kura na kuhamasishana kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura tarehe 29 Oktoba,2025  ili kuichagua CCM na viongozi wake wote kwa ushindi wa kishindo.

Matukio Mbali mbali kwa Picha katika uzinduzi huo.

                                           
                                   

Na Alifu Abdul Singida Iramba

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments