Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Martha Mlata, aliongoza mkutano huo na kuwataka wananchi kuendelea kumuamini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, ambaye ameonyesha uongozi thabiti unaojali wananchi, kusimamia amani, na kuendeleza maendeleo katika sekta mbalimbali.
Mlata pia alimuombea kura Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Singida Mjini, Yagi Kiaratu, akisisitiza kuwa ni kiongozi mwenye upeo, ari na nia ya kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo hilo. Aidha, alihimiza wananchi kuwachagua madiwani wote wa CCM ili kuimarisha mshikamano wa chama na kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Katika tukio hilo, hata watia nia waliowahi kushiriki mchakato wa kura za maoni walijitokeza hadharani kuunga mkono wagombea walioteuliwa, jambo lililoonyesha mshikamano, mshikikano na mshikamano wa kweli ndani ya CCM.
Hali hiyo iliwapa wananchi matumaini mapya kuwa ushindi wa CCM katika jimbo hilo ni wa kishindo.
Mkutano huo ulihudhuriwa pia na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, ambaye pamoja na watia nia wote, waliungana kumuombea kura Rais Samia Suluhu Hassan na Mgombea Ubunge Yagi Kiaratu, wakisisitiza kuwa ni chaguo sahihi kwa maendeleo ya Singida Mjini.
Picha Za Matukio Mbali Mbali Katika Mkutano Huo.

0 Comments